BREKING NEWS: MANJI AACHIWA KWA DHAMANA
DAR ES SALAAM: Mfanyabiashara maarufu nchini na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusufu Manji amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka moja la kutumia dawa za kulevya.
Akisoma shtaka hilo, wakili wa serikali, Mutalemwa Kishenyi alisema kuwa, Manji anashtakiwa kwa kosa moja la kutumia madawa ya kulevya aina ya heroine ambapo mshtakiwa alikana mashtaka hayo.
Baada ya kusomewa shtaka hilo, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeya alisema kuwa kutokana na kosa hilo, dhamana iko wazi kwa mshtakiwa endapo atakamilisha masharti.
Manji alikamilisha masharti chini ya wakili wake, Alex Mngongoro na kufanikiwa kupata dhamana ya bondi ya shilingi milioni 10 aliyodhaminiwa na Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa.
Aidha kesi hiyo imepangwa kutajwa tena mahakamani hapo,Machi 16, 2017.

Post a Comment