Video: Baada ya kuitwa nyani, Hamorapa atoa maneno mazito kwa Iyobo
Mose Iyobo, Dancer Kiongozi wa WCB ya Diamond Platnumz.
DANSA mashuhuri kutoka lebo kubwa Bongo ya Wasafi Classic
Baby (WCB) ambaye pia ni mzazi mwenza wa Anti Ezekiel, Mose Iyobo,
amefunguka kupitia mtandao wa ‘Tweeter’ wa Hamis Mandi Mtangazaji wa
XXL ya Clouds FM baada ya Bdozen ‘Hamis’ kuweka picha akiwa na mtafiti
wa wa Nyani (Sokwe) duniani, Jane Goodall, ambapo (Iyobo) alimtaka
mtafiti huyo apewe taarifa za uwepo wa nyani mwingine aitwaye Harmorapa.“Duh, noma sana ila mwambie kuna nyani anaitwa Harmolapa, angekuja kumfanyia utafiti na kujua tabia zake angetisha sana,” aliandika Mose Iyobo miongoni mwa Tweets za post hiyo.
Hamis Mandi (kulia) na Mchunguzi wa Nyani duniani, Jane Goodall.
Haijafahamika sababu ya Iyobo kumuita hivyo Harmorapa jina la mnyama,
kitendo kinachotafsiriwa kama ni dharau au huenda ipo tofauti kati yao.
Hamorapa, dogo aliyefananishwa na nyani.
Post a Comment