ad

ad

Breaking News: Waliofukiwa na Kifusi Mgodini Geita Waokolewa Wote (Picha zao zipo Hapa)




WATU 15 waliofukiwa kwa kifusi katika mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya Nyarugusu mkoani Geita, wameokolewa wote wakiwa hai kutokana na  jitihada zilizofanywa na wataalamu wa mgodi huo na mingine kwa kushirikiana na serikali.

 Habari zilizotufikia punde ni kwamba watu hao wameokolewa baada ya kukaa takribani siku tatu ndani ya mgodi bila kupata chakula na bila kuona mwanga wa jua.

Aidha, taarifa za awali zinasema kuwa baada ya kuokolewa watu hao  wamewekwa chini ya uangalizi wa karibu na wataalamu wanaendelea na uchunguzi huo ambapo baada ya muda itatolewa ripoti kamili.

No comments

Powered by Blogger.