Mrembo Atikisa Mitandaoni Bongo! Wema, Sanchi Kazi Wanayo! Check Picha zake hapa
Mrembo Sasha Kassim
DAR ES SALAAM: Mrembo aliyedai mwenyewe kuwa yeye
ndiye mvaa taji la Miss Lake Zone na Miss Mara, 2014 na kujitambulisha
kwa jina la Sasha Kassim (pichani), hivi karibuni alitupia picha zake za
nusu utupu kwenye mtandao lakini kubwa kuliko zote, ni mtikisiko
uliotokea kwenye jamii juu ya picha hizo, Risasi Jumamosi linatembea na wewe msomaji.MWONEKAKO WA PICHA
Baadhi ya picha zinamwonesha Sasha akiwa katika mapozi mbalimbali na nguo fupi za kupitiliza au bila nguo hali iliyoibua maneno kwamba aliyetupia picha hizo ni yeye mwenyewe kwa raha zake bila kujali taji la Miss Lake Zone analoshikilia kama alivyosema.
Mrembo Sasha Kassim, katika pozi
Picha nyingine zinamwonesha Sasha kama mrembo mwenye umbo ‘matata’ la
namba nane kiasi cha kuwaweka roho juu, warembo wenye majina makubwa
Bongo kama Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na modo mkali aliyeibuka siku za karibuni, Jane Ramoy ‘Sanchoka’. “Mh! Wema na yule modo, Sancha Sanchoka) wakae sawasawa, mtoto anakuja kwa moto huyu.Nadhani aliamua kutupia picha kwa sababu anajijua ana umbo la mtego,” baadhi ya wachangiaji walisema. Wema na Sancha wanaaminika kuwa ndiyo warembo wenye maumbo matata Bongo licha ya kuwepo wengine ambao nyota zao hazishaini katika eneo hilo. Wote hao (Wema na Sancha) wamewahi kuhusishwa na matumizi ya dawa za Mchina katika kukuza makalio yao, madai ambayo, wote wamekuwa wakikanusha vikali, tena Wema akisaidiwa na mama yake mzazi, Mariam Sepetu.Lakini picha za Sasha ambazo msomaji mmoja alizifikisha baadhi yake kwenye Ofisi za Global Publishers, zimeibua mjadala mkubwa hasa kuhusu figa yake kwamba, anaweza kuwa mrembo mwenye mvuto mkubwa kwa mwaka 2017.
RISASI JUMAMOSI LAMBANA SASHA
Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi, Sasha alisema watu wengi hawamuelewi na wanamchukulia tofauti baada ya kusambaa kwa picha hizo ambazo nyingi anaziweka mwenyewe kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.
ANAJIUZA?
Sasha alizidi kusema kuwa, baadhi ya watu wanamfikiria kuwa yeye anavyotupia picha hizo mtandaoni anajiuza au ni mwanamke asiye na maadili lakini kwa upande wake kufanya hivyo ndi yo maisha aliyolelewa.
BONYEZA HAPA KUMSIKIA MWENYEWE
“Unajua mimi si changudoa wala msichana asiye na maadili kama wanavyodhani. Mimi nimelelewa maisha ya Kizungu na hobi yangu kubwa ni kupiga picha hivyo watu wanaonifikiria vibaya wanajisumbua. Mimi siko hivyo kabisa,” alisema Sasha.
ETI FAMILIA YAKE INAMKUBALI
Akaendelea: “Kitu kikubwa ninachoangalia mimi ni kwamba, familia yangu inanipokeaje kwenye picha ninazopiga na mavazi ninayovaa? Basi. Lakini si mtu wa nje ambaye hanijui kiundani anasemasema tu.”MASWALI MACHACHE
Risasi Jumamosi: “Sasha, eti wewe ni Miss Lake Zone na Miss Mara mwaka gani?” Sasha: “Mwaka elfu mbili na…”
Risasi Jumamosi: “Mwaka elfu mbili na kumi na tano?”
Sasha: “Ndiyo, sikia, nipo na watu nitakucheki baadaye kwenye WhatsApp nitakutumia mwaka nilioshiriki.”
Risasi Jumamosi: “Poapoa.”
Mrembo Sasha Kassim, katika moja ya pozi zake
WAANDAAJI WA MISS TANZANIA WABEBESHWA NENOBaada ya kusambaa kwa picha hizo, baadhi ya watu waliutupia lawama uongozi wa juu unaoandaa mashindano ya Miss Tanzania, hasa bosi mkuu, Hashim Lundenga ‘Anko’ wak
isema huwa, wamekuwa wakibeba washiriki ambao hawana sifa kwa maana ya tabia, hasa uadilifu. Walisema kama kweli Sasha ni Miss Lake Zone basi ni miongoni mwa matunda hafifu ya uchaguzi wa washiriki wa mashindano hayo.RISASI JUMAMOSI NA MUANDAAJI WA MA-MISS
Ili kupata uhakika wa madai ya Sasha mwenyewe kwamba amewahi kushiriki Miss Lake Zone kwa mwaka uliosikika kuwa ni 2015, Risasi Jumamosi lilimtafuta muandaaji wa Miss Lake Zone, Flora Lauwo ambaye aliposomewa jina la mrembo huyo na mwaka wa kushiriki kwake, alisema: “Kwanza kabisa mwaka 2015 mashindano ya Miss Tanzania hayakuwepo, yalifungiwa na serikali kwa mwaka mmoja. Mimi niliandaa mwaka 2014 nikaandaa na mwaka 2016. Lakini hilo jina silikumbuki kabisa kwenye kumbukumbu yangu. Sasha?” Risasi Jumamosi: “Sasha ndiyo.” Flora: “Mh! Silikumbuki kabisa.”
Mrembo Sasha Kassim, katika moja ya pozi zake matata mitandaoni
RISASI JUMAMOSI NA MAJALIWA
Pia, Risasi Jumamosi likamsaka mmoja wa wanakamati wa Miss Tanzania ngazi ya taifa, Bosco Majaliwa ‘Mshua’ kwa kumtumia picha moja ya Sasha kama anamkumbuka, alisema hamkumbuki mrembo kama huyo kushiriki Miss Lake Zone.
RISASI JUMAMOSI NA LUNDENGA
Baada ya kumalizana na Majaliwa, Risasi Jumamosi likamsaka Anko Hashim na kuzungumza naye kwa njia ya simu kuhusu Sasha.
Lundenga: “Sasha?”
Risasi Jumamosi: “Ndiyo, anaitwa Sasha. Alishiriki Miss Mara na baadaye Miss Lake Zone ambaye anakuwa na sifa ya kuwa mshiriki wa Miss Tanzania.”
Lundenga: “Mimi namjua mrembo mwenye jina hilo ni Sasha Adam, yeye ni Miss Singida. Amefanya nini huyo Sasha unayeniulizia wewe?”
Risasi Jumamosi: “Kuna picha chafu anazitupia kwenye mtandao.”
Lundenga: “Mh! Hebu ngoja nitafuatilia kama kuna jina hilo kwenye Lake Zone, lakini sidhani.”Imoooo!
RISASI JUMAMOSI NA SASHA TENAKama ahadi yake ilivyosema kuwa, atatuma mwaka alioshiriki Miss Lake Zone, kweli, kabla gazeti hili halijaenda mitamboni, Sasha alituma kwa WhatsApp kwamba, mwaka 2014 ndiyo alishika taji la Miss Lake Zone lakini na kama muandaaji, Flora Lauwo alivyosema, hakumbuki kuwepo kwa jina hilo.
TCRA YATOA NENO
Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi aliwahi kuzungumza na gazeti hili na kusema kuwa, watu, wakiwemo wenye majina makubwa waache kutupia picha chafu kwenye mitandao kwa sababu, picha ikishaingia huko, hudumu miaka na miaka na inakuwa si mali ya aliyeitupia. Lakini akasema sheria inaruhusu Jeshi la Polisi Tanzania kuwakamata watu wanaofanya hivyo.
IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI
Post a Comment