Mo mwanaume bwana! anasepa na kijiji chake
SIMBA juzi ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, kwenye mchezo wake wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda lakini kiungo wao Mohamed Ibrahim maarufu kama Mo alionyesha moto wa hali ya juu. Ibrahim ambaye alisajiliwa na Simba akitokea kwenye kikosi cha Mtibwa Sugar alionyesha pia uwezo wa juu kwenye michezo ya mzunguko wa kwanza, lakini kiwango cha wikiendi iliyopita kilikuwa hatari zaidi. Kiungo huyo matata mara
kwa mara alikuwa akiwakusanya mabeki wa Ndanda (yaani kama anaondoka na kijiji kizima) na mashabiki kulipuka kwa shangwe. Kuna wakati aliuchukua mpira kutoka katikati akawa anakwenda kushoto akampunguza beki mmoja, wa pili, wa tatu, ghafla akawa analindwa na mabeki wanne wa Ndanda hali ambayo ilimfanya akautoa mpira huku mashabiki wakimshagilia. Kocha mmoja wa soka nchini ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alisema kuwa aina ya mchezaji huyu ya kucheza ni ya hali ya juu na kama Simba watamtunza vizuri, basi atakuwa
hatari sana misimu kadhaa ijayo.
“Ni wachezaji wachache sana wanaweza kucheza kama huyu hapa nchini, unajua wengi huwa hawamuangalii vizuri, lakini ana staili ya pekee, ni wachache sana wanaweza kuondoka na mpira kwa kasi, halafu akasimama wengi wakifikiri anatoa pasi halafu akaondoka tena kwa kasi ileile
“Huyu amekuwa akifanya mara kwa mara, kama unataka kuamini angalia mechi ijayo ya Simba, halafu huwezi kumkaba kirahisi kwa kuwa hujui atapitia wapi,” alisema kocha huyo. Mo kwa sasa ana mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara kuanzia amejiunga na Simba.

Post a Comment