ad

ad

Mkata Umeme wa Yanga ruksa kukipiga

RASMI! Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa tayari kuanza kumtumia kiungo wao mpya, Justine Zulu maarufu kama Mkata Umeme na Ijumaa wiki hii atakata mawasiliano ya African Lyon kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. 
 
Mzambia huyo wiki iliyopita alilazimika kukaa jukwaani wakati Yanga ikiinyuka JKT Ruvu mabao 3-0 kwa kile kilichofafanuliwa kuwa ni kuchelewa kwa kibali chake cha kuishi nchini ‘residency permit’ ambacho tayari wamepewa.

 Katibu wa Yanga Baraka Deusdedit amelifafanulia zaidi Championi Jumatano kikwazo
 kilichomfanya Zulu kuondolewa kwenye ‘line up’ kabla ya mechi kuanza na nafasi yake kuchukuliwa na Said Juma Makapu.


 “Mpaka Ijumaa, siku moja kabla ya mchezo, Zulu tayari alikuwa na ITC (Hati ya Uhamisho) na cha kufanya kazi nchini ‘work permit’, tatizo lilikuwa ni kibali cha kuishi ambacho ni moja ya vitu muhimu kuhakikisha awe navyo, kilichotokea ilishindikana kukipata.

 “Lakini kila kitu tayari na Ijumaa wale wenye hamu ya kumuona akicheza basi ni wakati wao maana tumekamilisha taratibu zote zinazohitajika na kibali hicho kilichomkwamisha kimeshafika,” alisema katibu huyo.

No comments

Powered by Blogger.