ad

ad

HATIMAYE AZAM FC YATHIBITISHA KUONDOKA KWA KIUNGO WAKE MNYARWANDA



Baada ya gazeti la Championi kuandika kiungo Jean Baptiste Mugiraneza hatarejea Azam FC, uongozi wa klabu hiyo umelithibitisha hilo.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amesema Mugiraneza raia wa Rwanda alibaki mkataba wa miezi sita ambao wameununua.

“Amekubali, tumeununua mkataba na yeye ameondoka kwenda Vietnam ambako amepata timu ya kuichezea,” alisema Iddi.

Mugiraneza alijiunga na Azam FC akitokea APR ya Rwanda ambayo aliichezea kwa mafanikio makubwa kwa zaidi ya misimu minne.

No comments

Powered by Blogger.