AZAM FC SASA RASMI, YAWASAINISHA MAHUNDI, MPONDO NA YAKUBU
Uongozi
wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unayofuraha
kuutarifu umma kuwa leo mchana imefanikiwa kuingia mkataba na wachezaji
watatu, beki wa kati Yakubu Mohammed, kiungo mkabaji Stephan Kingue
Mpondo na winga Joseph Mahundi.
Zoezi
hilo la kuingiana mikataba limehudhuriwa na baadhi ya viongozi wakuu wa
timu wakiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, Meneja Mkuu, Abdul
Mohamed, Kocha Mkuu Zeben Hernandez, Meneja wa timu, Phillip Alando.
Wakati
Mohammed, 20, amesaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Aduana Stars ya
Ghana, utakaomuweka kwenye viunga vya Azam Complex hadi Desemba 14,
2019 akiziba nafasi ya Pascal Wawa, huku Mpondo anayetokea Coton Sports
ya Cameroon, kwa upande wake akisaini mwaka mmoja.
Nyota
hao wawili wamepewa rasmi mikataba baada ya kulivutia benchi la ufundi
la Azam FC kwenye majaribio waliyokuwa wakifanya ndani ya kikosi hicho.
Katika
kuongeza makali kwenye eneo la ushambuliaji, Azam FC imemrejesha winga
wake wa zamani aliyekulia Azam Academy, Mahundi, ambaye amesaini miaka
miwili akitokea Mbeya City, alipomaliza mkataba baada ya kumalizika kwa
raundi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Azam
FC tunaamini ya kuwa ujio wa nyota hao, utazidi kuipa nguvu timu yetu
kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL)
unaotarajia kuanza wikiendi hii, Kombe la Shirikisho (Azam Sports
Federation Cup) na Kombe la Shirikisho Afrika (CC) mwakani.
Hivyo
mashabiki wa Azam FC wasiwe na wasiwasi waendelee kuisapoti timu, kwani
bado uongozi wa timu kwa kushirikiana na benchi la ufundi, una nia ya
dhati ya kuipeleka mbele timu kufikia kwenye mafanikio yanayokusudiwa
kwa kukiboresha kikosi kadiri inavyowezekana.
Wakati
huo huo, Azam FC inapenda kuweka wazi taarifa ya kufikia makubaliano ya
kuachana na kiungo mkabaji raia wa Rwanda, Jean Baptiste Mugiraneza
‘Migi’, ambaye amepata timu nchini Vietnam na muda wowote kuanzia sasa
atakwenda huko.
Azam
FC inamtakia mafanikio mema Migi huko aendako na inapenda kumkaribisha
muda wowote atakapojisikia kurejea tena hapa na katika kuziba nafasi
yake tumeamua kumsajili Mpondo, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya Taifa
ya Cameroon kwenye kikosi kilichoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika
kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizofanyika nchini Rwanda mwanzoni mwa
mwaka huu.
Post a Comment