EXCLUSIVE: NGASSA ASAFIRI KIMYAKIMYA KWENDA MBEYA, ANAWEZA KUMALIZANA NA MBEYA CITY
| NGASSA AKIWA NDANI YA NDEGE KWENDA MBEYA, LEO. |
Mrisho Ngassa leo amekweda pipa la Fastjet kwenda mjini Mbeya ambako inaelezwa atamalizana na klabu ya Mbeya City.
Ngassa ambaye hivi aliachana na Free
State Star ya Afrika Kusini na kwenda kujiunga na Fanja ya Oman ambako
aliondoka na kurejea Dar es Salaam kimyakimya.
Dirisha la usajili linafungwa kesho na
taarifa za ndani kutoka Mbeya City zimeeleza, mazungumzo kati ya Ngassa
na Mbeya City inayonolewa na Kocha Mmalawi, Kinnah Phiri yanakwenda
vizuri na huenda leo au kesho wakamalizana.
Phiri ndiye alimsajili Ngassa Free State, lakini siku chache kocha huyo aliondoka katika klabu hiyo ya Afrika Kusini.
Kama atasaini kujiunga na Mbeya City
itakuwa ni timu yake ya sita kuichezea katika Ligi Kuu Tanzania Bara
baada ya Toto African, Kagera Sugar, Yanga, Azam FC na Simba.

Post a Comment