Singidani (A Story From My Heart) - 11

ILIPOISHIA...
Chris akalipa kisha akaondoka zake na kwenda kuchukua taksi nyingine iliyompeleka Kibaoni, ambapo ndipo gesti iliyokuwa na begi lake na vitu vyake vingine. Gari liliingia eneo hilo na kuegesha mbele ya geti.

“Naomba ukaniitie mhudumu
tafadhali,” Chris akamwomba yule dereva ambaye alitii.
Sekunde chache sana baadaye, Mwanjaa alitokea, akakutana na swali kutoka kwa Chris: “Vipi, jamaa walirudi tena jana?”
Chris alisubiria jibu la Mwanjaa akiwa mwenye wasiwasi mwingi sana. Bado hakujua hatma yake.
SASA ENDELEA....

WASIWASI ulimjaa moyoni akiwa hajui
kabisa kilichotokea usiku wa kuamkia siku hiyo. Macho yake aliyatuliza usoni
mwa Mwanjaa akisubiri kusikia jibu lake. Mwanjaa alionekana kusita kidogo.
“Vipi... walikuja? Naomba uniambie haraka maana natakiwa kuondoka.”
“Hapana,” Mwanjaa akajibu.
“Asubuhi hii?”

“Pia hawajaja.”
“Sikia... naomba unichukulie begi langu pale ndani, kuna vitu vyangu vingine vidogovidogo vipo kwenye kabati.”
“Sawa kaka.”
Mwanjaa akatoka haraka na kwenda ndani. Dakika tatu baadaye, alitoka ndani akiwa na begi la Chris. Ghafla Mwanjaa akaonekana kusimama na kuonyesha kuwa na mshangao mkubwa sana.

Chris alipoangalia barabarani,
akashtuka sana baada ya kuwaona maaskari wanne wenye silaha wakivuka mfereji
mdogo uliokuwa pembeni mwa barabara kuu ya Dodoma – Mwanza. Pembeni waliegesha
karandinga lao. Kufumba na kufumbua, taksi ilikuwa imezungukwa na maaskari
wale.
“Nimekwisha!” Chris akajisemea moyoni.
“Hamtakiwi kufanya chochote kwa sasa,” mmoja wa maaskari wale akasema.
“Tumefanya nini?” Chris akauliza.

“Haya mikono juu,” akasema yule
askari.
Wakafanya hivyo.
Maaskari wawili kati yao, waliingia garini na kuanza upekuzi, baadaye wakamuamuru dereva afungue buti. Wakakagua lakini pia hawakuona walichokuwa wakikitafuta ambacho pia hawakusema ni nini.
“We’ dada, hiyo mizigo ni ya nani?” mmoja wao akauliza.
“Wa huyo hapo...” Mwanjaa akajibu haraka akimsonza kidole Chris.
“Lete.”

Mizigo ikapelekwa.
Haraka ikaanza kukaguliwa, Chris alikuwa akipewa maelekezo na kuambiwa atoe nguo moja baada ya nyingine na vitu vingine vilivyokuwa ndani ya begi lake.
“Wewe unaitwa nani?”
“Naitwa Dk. Christopher.”
“Unatokea wapi?”
“Dar es Salaam.”

“Unaelekea wapi?”
“Nakwenda Kiomboi,” akadanganya Chris.
“Tunaweza kuona kitambulisho chako?”
“Bila shaka.”
Mara moja Chris akatoa na kuwapa. Wasiwasi ulikuwa moyoni lakini kwa namna fulani ulianza kuondoka akiwa na imani kuwa walichokuwa wakikifuatilia kwake hakikuwa kuhusu Laura tena.

Wakakagua kitambulisho chake kisha
wakamrudishia.
“Wewe dada ni nani?” askari mmoja akamwuliza Mwanjaa.
“Mhudumu.”
“Nahitaji kuona kitabu chako cha wageni,” akasema yule askari akiongozana na Mwanjaa ndani.
Alipofika getini yule askari ambaye alionekana ndiye kiongozi wao, aligeuka na kusema: “Ninyi mnaweza kwenda.”
Chris akaingia kwenye gari, dereva akawasha moto, akaondoa gari.
***
Maswali yalikuwa mengi kuliko majibu, lakini jambo kubwa kwa Chris wakati ule ni kwamba alikuwa amefanikiwa kuondoka mikononi mwa hatari ya kuingizwa kwenye kashfa ya kutembea na mke wa mtu. Yaliyoendelea nyuma hayakuwa na maana kwake.
Ndani ya Basi la Beffe, Chris alikuwa kimya kabisa, akitafakari mtihani wake uleule; kwenda kuoa kijijini.
***
Laura alikuwa akitengeneza nywele zake saluni iliyokuwa Ginnery. Hisia zake za ndani bado ziliendelea kumhakikishia kuwa Chris ndiye angekuwa mwanaume wa maisha yake. Hakutaka kusikia mwanaume mwingine zaidi yake.
Alijiuliza, kwanini hakupokea simu yake? Kwanini hakuonekana klabu kama walivyokubaliana? Kwanini hapatikani hewani?

“Kwanini naingia kwenye mateso
makubwa kiasi hiki? Nampenda Chris, nina hakika na hisia zangu. Sikutegemea
kama hili lingetokea kirahisi hivi, lakini inanipasa nikubali kuwa nimeshatekwa
na ninampenda. Nitahakikisha nampata Chris, lazima,” aliwaza Laura.
Itaendelea .
Itaendelea .
Post a Comment