Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kufanya Ziara Ya Kikazi Mkoani Arusha

Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MHE. Kassim Majaliwa
anatarajiwa kutembelea Jiji la Arusha kuanzia kesho tarehe 01 hadi
03/12/2016 na kukagua miradi ya maendeleo, kuongea na watumishi wa Jiji,
kukutana na wafanyabiashara pamoja na kuzungumza na wananchi.
Kwa
mujibu wa Afisa habari wa Jiji la Arusha Nteghenjwa Hosseah, kesho
tarehe 01/12/2016 Waziri mkuu MHE. KASSIMU MAJALIWA atatembelea National
Milling Company (NMC) na pia atakagua ujenzi wa barabara ya Friends
Corner - Muriet yenye urefu wa Km 7 inayojengwa kwa kiwango cha Lami
kupitia mradi wa Mpango Mji Mkakati (TSCP) na kusimamiwa na Ofisi ya
Rais Tamisemi.
Hosseah
amesema siku ya tarehe 02/12/2016 Waziri Mkuu atakutana na kuzungumza
na watumishi pamoja walimu katika Ukumbi wa AICC Arusha na baadae
atakutana na wafanyabiashara katika Ukumbi huo.
"Katika
nsiku ya tatu ya ziara yake Mhe Majaliwa atatembelea na kukagua
viwanda vya Lodhia pamoja na Hans Paul vilivyoko mtaa wa Viwanda – Njiro
na baadae atakutana na wanachi wote kwenye Mkutano wa hadahara
utakaofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuanzia saa nane
mchana."
Post a Comment