Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Singida Afariki Dunia Muhimbili

Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) EX Peter Kakamba amefariki dunia alfajiri ya tarehe
30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa
matibabu.
Kakamba
alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa
wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense mwaka 1973 hadi
1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari
Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma
katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987.
Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Marehemu
alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake
alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti
wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi
(2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008),
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015)
na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
Baadhi
ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mwendesha Mashtaka wa
Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa
mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa
wa Singida.
Kufuatia
kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole
kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi
Post a Comment