Muhimbili yakusanya Sh. bilioni 4.6
Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano ya umma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligaesha akizungumza na wanahabari
Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili imeongeza mapato yake kwa asilimia 100 baada ya kukusanya
jumla ya shilingi bilioni 4.6 ukilinganisha mwaka jana ambapo walikusanya sh.
Bilioni 2.3.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano ya Umma katika hospitali hiyo, Aminiel Aligeisha imesema:
“Baada ya
kuongeza kasi ya usimamizi wa wafanyakazi na kupunguza kero za weafanyakazi,
hospitali imeongeza uzalishaji wenye tija kwa kiwango kikubwa ambapo takwimu
zinaonesha kuwa kuanzia Desemba 2015 hadi Oktoba 2016 hospitali ilizalisha
wastani wa kiasi cha shilingi bilioni 4.6 kwa mwezi kutoka wastani wa shilingi
bilioni 2.3 iliyokuwa ikizalishwa kwa kipindi kama hicho cha Desemba 2014 hadi
Oktoba 2015.”
Alisema hayo
ni mafanikio makubwa kwa upande wa
mapato kuwahi kupatikana katikakipindi kifupi sana cha miezi miwili tu.
Aliongeza
kuwa hospitali kwa sasa kulingana na uzalishaji unaoonekana, inajitahidi
kupunguza madeni iliyonayo kwa wazabuni mbalimbali wakiwemo wanaoanyia matengenezo
kinga ya vifaa tiba vya hospitali.
Kuhusu
upatikanaji wa dawa, Aligaesha alisema kwa sasa wagonjwa wanapata dawa kwa
zaidi ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya dawa ya hospitali na tiba kwa wagonjwa
wanaofanyiwa kliniki inaanza saa tatu asubihi.
Post a Comment