Mtoto Mchanga ‘Azaliwa’ Mara Mbili
MTOTO
mchanga wa kike kutoka Lewisville, Texas, ‘amezaliwa’ mara mbili baada
ya kutolewa katika kizazi cha mama yake kwa dakika 20 ili kufanyiwa
upasuaji.
Akiwa na ujauzito wa miezi minne,
Margaret Hawkins Boemer aligundua kuwa binti yake, Lynlee Hope, ana
uvimbe katika uti wake wa mgongo.
Uvimbe
huo unoajulikana kama sacrococcygeal teratoma, ulikuwa unasukuma damu
kutoka kwa mtoto huo, jambo lililoongeza hatari ya moyo wa mtoto huyo
kutofanya kazi.
Baby Lynlee alikuwana uzito wa chini ya kilo moja wakati wapasuaji walipomtoa kwenye uzao wa mamake.
Bi Boemer awali alikuwa amebeba mimba ya
pacha, lakini alimpoteza mtoto mmoja kabla ya kumaliza miezi mitatu ya
kwanza. Awali alishauriwa kuitoa mimba hiyo kabla ya madakatari wa wa
hospitali ya watoto ya Texas Children’s Fetal Center kumpndekezea
upasuaji huo wa hatari.
Uzito wa uvimbe huo na ule wa mtoto
ulikuwa karibu sawa wakati upasuaji ulipofanywa. Aliarifiwa kuwa mwanawe
Lynlee ana asilimia 50 ya kufanikiwa kuishi.
Bi Boemer aliambia CNN: ” nikiwa na
miezi mitano, uvimbe huo ulikuwa unasitisha moyo wake kufanya kazi,
kwahivyo ilikuwa ni uamuzi baina ya kuruhusu uvimbe huo ummalize au
kumpa nafasi ya kuishi.
“Ulikuwa uamuzi wa rahisi kwetu: Tulikuwa tunataka kumpa maisha.”
‘Moyo wake ulisiti kupiga’
Upasuaji
Daktari Darrell Cass wa Texas Children’s
Fetal Centre nimojawapo ya matabibu waliotekeleza upasuaji huo. Amesema
uvimbe huo ulikuwa mkubwa, kiasi cha kuhitaji upasuaji mkubwa kuufikia,
jambo lililohatarisha maisha ya mtoto huyo.
Moyo wa Lynlee nusra usite kupiga wakati
wa upasuaji huo lakini mtaalamu wa moyo alimsaidia kuendelea kuishi
wakati uvimbe huo ulipakuwa unatolea, aliongeza.
Madaktari hao baadaye walimrudisha katika uzao wa mamake na kuufunga uzao kwa kuushona.
Bi Boemer alisalia kitandani kwa wiki 12 zilizofuata, na Lynlee alizaliwa kwa mara ya pili mnamo Juni 6.
Alizaliwa kwa upasuaji akiwa aribu kutumiza miezi tisa tumbano, na alikuwa na karibu kilo mbili na nusu.
Lynlee alipofikisha siku nane baada ya kuzaliwa, alifanyiwa upasuaji mwingine kutoa uvimbe uliosalia katika uti wake wa mgongo.
Dr Cass anasema mtoto huyo sasa amerudi nyumbani na anaendelea vizuri.
“Bado ni mchanga lakini anaendelea vizuri,” amethibitisha.
Sacrococcygeal teratoma ni uvimbe usiojitokeza sana na huwapata watoto 30,000 kati ya 70,000 wanaozaliwa.
Haijulikani husababishwa na nini lakini watoto wa kike huathirika mara nne zaidi kuliko wavulana.
Post a Comment