MTIHANI WA KWANZA KWA MWAMBUSI LEO, AIKANA PRISONS, NGUVU NI KWA JKT RUVU UWANJA WA UHURU
Kocha
Juma Mwambusi ndiye ataiongoza Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara
dhidi ya Ruvu JKT kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo.
Mwambusi tayari amesema, hana mpango wa kuhamia Prisons na wala hajajiuzulu Yanga kama ambavyo imeelezwa.
Akili yake anaielekeza katika mechi ya leo na lengo kubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi hiyo.
Yanga
inaivaa JKT ikiwa bila ya kocha wake, Hans van der Pluijm ambaye
amebwaga manyanga baada ya George Lwandamina kutoka Zambia kufika nchini
na kuzungumza na Yanga.
Aidha,
Kocha wa JKT Ruvu, Malale Hamsini, ameibuka na kuwatambia wapinzani wao
Yanga kwa kusema kuwa wasifikiri watapata mteremko katika mchezo wa
leo.
Yanga
leo inavaana na JKT Ruvu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika
Uwanja wa Uhuru jijini Dar, ikiwa imetoka kuwachapa Kagera Sugar mabao
6-2.
Kocha
Mkuu wa JKT Ruvu, Malale Hamsini, amesema kuwa, siyo mara ya kwanza
kukutana na Yanga, hivyo wasifikirie watapata mteremko kutokana na
kuwafunga Kagera Sugar mabao 6.
“Kikosi
chetu kipo vizuri na timu ipo kambini, hakuna majeruhi hata mmoja zaidi
ya Michael Aidani aliyekuwa majeruhi wa muda mrefu lakini kwa sasa
ameshaanza mazoezi.
“Lakini
Yanga wasitegemee mteremko kwa kupata matokeo mazuri kwetu kutokana na
kuifunga Kagera Sugar mabao sita kwani tumejiandaa vizuri kwa ajili ya
mechi hiyo.
“Siyo
mara yetu ya kwanza kukutana na Yanga, hivyo tunaiona ni timu ya
kawaida na kikosi chetu kipo vizuri kwa ajili ya kupambana nao,” alisema
Malale.
Post a Comment