YANGA KUANZA LIGI NA AFRICAN LYON LEO UWANJA WA TAIFA, DANTE NDANI, KIKOSI CHA YANGA HIKI HAPA
Kwa
mara ya kwanza Yanga itakuwa ikikanyaga nyasi za Uwanja wa Taifa, leo
Jumapili kukipiga dhidi ya African Lyon katika msimu wa 2016/17.
Huu
utakuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga kwa kuwa ilikuwa bize na michuano ya
kimataifa ambapo ilikuwa ikishiriki katika Kombe la Shirikisho Afrika
baada ya kushushwa hapo ikitokea michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Salehjembe
itakuletea matukio yote kuanzia dakika ya kwanza mpaka mchezo
utakapomalizika ‘LIVE’. Tayari kikosi cha Yanga kimejulikana kuelekea
katika mchezo huo, nacho ni hiki hapa:
1. Deo Munishi ‘Dida’
2. Hassan Kessy
3. Haji Mwinyi
4. Andrew Vincent ‘Dante’
5. Vincent Bossou
6. Thaban Kamausoko
7. Simon Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Donald Ngoma
10. Amiss Tambwe
11. Deus Kaseke
Sub
Kakolanya, Oscar, Pato Ngonyani, Mahadhi, makapu, Mateo, Yusuph
Post a Comment