Diamond amtusi Wastara kisa studio ya WCB!
Diamond Platnumz
Tukio hilo lililopigwa chabo na chanzo
chetu lilijiri wikiendi iliyopita katika moja ya studio za runinga
ambapo Wastara alikwenda kumpeleka msanii wake aitwaye Ibrahim Khaan kwa
ajili ya mahojiano.
Sosi wetu aliliambia Wikienda kuwa,
Diamond alimshushia Wastara matusi kwa madai kuwa ni shabiki wa Ali Kiba
na kwamba kwa muda mrefu alikuwa akimsaka ili ampe makavu.
Wastara Juma.
CHANZO CHAFUNGUKA
“Jamani mimi nimemsikia kwa masikio yangu Diamond akimtukana Wastara matusi
ya nguoni, kisa ni ushabiki wake kwa Ali Kiba.
“Unajua Wastara ana msanii wake ambaye
‘anammeneji’, walipokuwa kwenye studio za runinga walikutana na meneja
wa Harmonize anayeitwa Momo.
“Huyo Momo anajuana na mdogo wa Wastara
hivyo walipoonana walisalimiana kisha akatokea Harmonize ambaye naye
alisalimiana na Wastara.
“Wastara ndiye aliyeomba kuonana na
Diamond kwa sababu msanii wake alikuwa akihitaji kubadilishana naye
mawazo,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, baada ya kuongea na Wastara,
Momo alimfuata Diamond kwenye gari akiwa ameongozana na mdogo wa
Wastara ambaye alimweleza Diamond kuwa Wastara alikuwa akitaka kuongea
naye.
Chanzo kiliendelea kusimulia kuwa
Diamond, alianza kutoa maneno mazito na kusema kwa nini asiende kwa Ali
Kiba kisha akatukana matusi mazito yasiyoandikika gazetini.
Chanzo hicho kilidai kwamba, wakati
Diamond akitoa lugha hiyo kali kwa Wastara, Harmonize alikuwa pembeni
hivyo aliinama kwa aibu.
WASTARA NA DIAMOND
Ilisemekana kuwa, Wastara alipomsogelea
Diamond alimsalimia Diamond ambaye aliitikia akiwa amekasirika kisha
Wastara akaanza kujieleza kuwa alikuwa akihitaji msanii wake akafanyie
kazi yake kwenye Studio za Wasafi.
Chanzo kilieleza kuwa Diamond aliendelea kumkejeli Wastara akimhoji kwa nini Wasafi na si kwa Ali Kiba?
Ilielezwa kuwa Wastara alicheka na kumwambia kuwa yeye amependa kurekodia Wasafi na nia yake si ushabiki bali ni kazi tu.
DIAMOND AKATISHA MAONGEZI
Hata hivyo, ilisemekana kwamba, Diamond hakutaka maongezi hivyo alimkatisha kwa kumwambia kuwa jambo hilo amalizane na Momo.
Baada ya habari hiyo kutua kwenye dawati
la Wikienda, mwanahabari wetu alimtafuta Wastara kwa njia ya simu
ambapo alikiri kukutana na Diamond na kuzungumza naye ishu za msanii
wake lakini hakujua kama kulikuwa na matusi.
“Sina ugomvi naye na wala hayo ya matusi
sijui ila ni kweli nilikutana naye na nilipanga kwenda kwenye studio
yake lakini alinihoji kuhusiana na kuichagua studio yake, nikamweleza
natafuta ubora na nitafanyia studio mbalimbali ikiwa ni pamoja na huyo
Ali Kiba,” alisema Wastara.
Wikienda lilimtafuta Diamond kwa njia ya
simu lakini jitihada za kumpata ziligonga mwamba baada ya kuita kwa
muda mrefu bila kupokelewa hivyo zinaendelea.
CHANZO: HAMIDA HASSAN, WIKIENDA/GPL
Post a Comment