YANGA YAFAFANUA KUHUSIANA SAKATA LA MKATABA WAO WA TBL, WAVUNJA MKATABA NAO
Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji jana ametoa ufafanuzi kuhusiana na suala la
mkataba wa klabu hiyo dhidi ya Kampuni ya Bia Tanzania.
Manji ameeleza ikiwa ni siku chache baada ya Yanga kuonekana wakiwa wamevaa jezi zenye nembo ya Quality Group badala ya Bia ya Kilimanjaro ambao wanajulikana ni wadhamini wao.
Yanga ilionekana kwa mara ya kwanza ikiwa imevaa jezi zenye nembo ya Quality Group wakati ikiivaa TP Mazembe katika mechi ya Kombe la Shirikisho na kupoteza kwa bao 1-0.
Katika taarifa yake, Manji ametoa ufafanuzi kuhusiana na mkataba huo.
MKATABA WA TBL NA YANGA

3.1. Mkataba
wa kampuni ya bia nchini (TBL) na YANGA ulisainiwa miaka mitano
iliyopita na mtangulizi wangu. Huu ulikuwa mkataba haramu kwani mamlaka
ya kutia saini mikataba kwa mujibu wa Katiba ya Yanga yapo kwa
wadhamini na hapana kitu kama azimio kutoka bodi ya wadhamini kuingia
katika makubaliano kama haya, au mkataba kusainiwa na wadhamini.
3.2. Wakati
wa kipindi changu kilichopita, nilijitahidi kurekebisha tofauti zote
zilizokuwepo, lakini nilishindwa. TBL ni mara moja tu imetoa mara moja
tu Sh. 20 Millioni kwa ajili ya tamasha la Yanga Day zilizoahidiwa
kutolewa kila mwaka, haijailipa klabu fedha ya marekebisho inayofikia
Sh. 30 Milioni wala haijatupa basi kwa kiwango sahihi tulichotaka kama
ililoahidi katika mkataba. TBL imejulishwa kuhusu hili lakini
haijalishughulikia.
3.3. Yanga
imeingia katika mkataba wa masoko na kampuni ya International Marketing
ili kupata wafadhili wake, ili kupunguza pengo la TBL kwa ajili ya
mishahara ya Juni. Hii ni kampuni ambayo nilikuwa mwenyekiti wake na
ikakubali ufadhili huo wa mwezi mmoja, jambo ambalo liliifanya Yanga
kuvaa jezi za nembo yake katika mchezo dhidi ya TP Mazambe.
3.4. Iwapo
wanachama wa Yanga wakihisi nilivunja katiba kwa maslahi yangu binafsi
au wakiwa na sehemu nyingine bora zaidi ya kufanya hivyo, walifikishe
suala hilo kwenye kamati ya maadili ya klabu kwa ajili ya uamuzi.
YUSUF MEHBUB MANJI
MWENYEKITI KLABU YA YANGA
YUSUF MEHBUB MANJI
MWENYEKITI KLABU YA YANGA

Post a Comment