Jini Kabula aswekwa lupango
Kibano! Staa wa sinema za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amejikuta kwenye mikono ya sheria na kuswekwa lupango baada ya kumtukana shosti yake, Miss Kinondoni 2009, Stella Mbuge.
Kwa mujibu wa mtoa ubuyu wetu makini,
Kabula alitaitiwa na polisi usiku wa Jumatano iliyopita mara baada ya
kutendo kosa hilo walipokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar
wakitazama mechi kati ya Yanga na TP Mazembe ya DR Congo.
“Walipishana kauli kule uwanjani, si
unajua Kabula ni Yanga damu, sasa nahisi alishindwa kustahimili utani wa
Stella ndipo akamporomoshea matusi ambayo yalimfanya mwenzake akimbilie
polisi.
“Alikwenda kushtaki Polisi Kijitonyama
(Mabatini), akapewa polisi na kwenda kumkamata Kabula ambaye wakati huo
alikuwa kwenye sherehe ya mtoto wa Esha Buheti. Wakamtia ndani hadi
kesho yake (Jumatano) walipomtoa kwa dhamana,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kunasa ubuyu huo, Jumatano iliyopita, Risasi Jumamosi lilimtafuta Kabula ili kumsikia anazungumziaje ubuyu huo ambapo alikiri kutokewa na tukio hilo na kudai wameshamalizana.
“Ni kweli ilikuwa hivyo lakini tumeshamalizana kiutu uzima, yamekwisha tayari,” alisema Kiba.
Alipoulizwa Stella, aliahidi kufafanua kwa ujumbe mfupi (SMS) tukio hilo lakini hadi tunakwenda mitamboni, hakutuma.
CHANZO:RISASI
CHANZO:RISASI

Post a Comment