Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry leo Atangaza kuwa kesho Jumatano ni Sikukuu ya Eid el Fitri
Kwa
 kipindi cha mwezi sasa waislamu walikuwa katika mfungo wa Mwezi Mtukufu
 wa Ramadhani wakitimiza  ibada ya nguzo za uislamu ambayo ni Kufunga.
Baadhi ya waislamu kutoka mataifa mbali mbali  wakiwepo wajerumani na Afrika magharibi, leo wamesherekea sikukuu ya Eid el fitr baada ya kumaliza mfungo wao.
Hata
 hivyo leo Mufti Mkuu wa tanzania Zubeir Bin Ally amewataka  pia waislam
 kujitokeza  kesho katika misikiti mbalimbali kwa ajili ya ibada ya Eid el Fitr.
Taarifa ambayo imetolewa leo ni uthibitisho wa  sikukuu ya Eid el Fitr ambapo Waislam wote walikua wakisubiri kuandama kwa mwezi.
Kwenye taarifa yake Muft Zubeir amesema Mwezi huo umeonekana sehemu mbalimbali za nchi yetu ya Tanzania, hivyo  kesho Jumatano ni Sikukuu ya Eid el Fitri 

Post a Comment