Kampuni ya mabasi ya City Boy iliyoua Watu 30 yafungiwa
Siku
 moja baada ya kutokea ajali ya mabasi iliyosababisha vifo vya watu 30 
na majeruhi kadhaa, Kampuni ya mabasi ya City Boy imefungiwa kufanya 
biashara hiyo kwa muda usiojulikana.
Ajali
 hiyo ilitokea eneo la Maweni, Manyoni, mkoani Singida baada ya mabasi 
ya kampuni hiyo, moja likitokea Dar es Salaam na lingine likitokea 
Kahama kuelekea Dar es Salaam kugongana.
Msemaji
 wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), 
David Mziray amesema leo kuwa kampuni hiyo ina miliki mabasi 12 na yote 
yamefungiwa kufanya safari yoyote kuanzia leo. 
“Mabasi hayo yamefungiwa kuanzia leo kwa muda usiojulikana, ukaguzi wa mabasi yao utaanza kufanyika kupitia jeshi la polisi,” amesema Mziray.

Post a Comment