RIDHIWANI KIKWETE AWEKA WAZI, KURA YAKE NI KWA MANJI
Shabiki
wa kugalagala wa Yanga, Ridhiwani Kikwete amesema amejitokeza kusema
wazi iwapo Yusuf Manji atachukua fomu kugombea tena nafasi ya
mwenyekiti, yeye atakuwa kati ya watakaompa kura.
Ridhiwani ambaye ni Mbunge wa Chalinze (CCM), amesema ameridhishwa na mafanikio iliyoyapata Yanga ikiwa chini ya Manji.
“Niwe
mkweli kabisa Yanga imekuwa na maendeleo mazuri chini ya uongozi wa
bwana Manji. Hili linanifanya kura yangu iwe kwake kama ataamua
kuendelea kugombea,” alisema Ridhwani.
Manji anatarajia kuchukua fomu leo katika uchaguzi ambao utafanyika Juni 11 jijini Dar es Salaam.

Post a Comment