Kajala hatarini kupata kansa daktari afunguka mazito!
STAA wa filamu Bongo, Kajala
Masanja, yupo hatarini kupata ugonjwa wa kansa, endapo ataendelea
kukiuka masharti aliyopewa na daktari wake juu ya matibabu ya matatizo
yake ya ubongo.
Chanzo kilicho karibu na staa huyo,
kimetonya kuwa baada ya matatizo yake kugundulika, daktari alimpa dawa
ambazo anapaswa kuzinywa saa moja usiku kila siku huku akitakiwa
kupumzika kwa muda mwingi, lakini badala yake amebadili muda na pia
anapiga ‘ulabu’.
“Kajala asipofuata masharti ya daktari
basi siku si nyingi tunaweza kumpoteza au kujikuta akipatwa na maradhi
makubwa zaidi. Alikatazwa kunywa pombe, lakini amemrubuni na
kubadilishiwa muda ili apate fursa ya kupiga mitungi.
“Alitakiwa kunywa dawa saa moja usiku,
ila ameshindwa, alimuomba daktari ambadilishie muda na kupewa saa 4
asubuhi,” kilisema chanzo hicho.
Inaelezwa kuwa wakati akiomba
kubadilishiwa muda, aliomba pia aruhusiwe japo ‘wine’ kidogo, jambo
ambalo daktari alimkubalia, lakini kwa sharti la angalau saa tatu kabla
hajanywa dawa, abugie maji lita tatu, kitu ambacho kimekuwa kigumu kwa
staa huyo kutokana na kubanwa na ratiba.
Alipotafutwa Kajala mwenyewe ili kuzungumzia hilo, alikiri:
“Ni kweli nilimwambia daktari
anibadilishie muda toka usiku na sasa natumia asubuhi, ninajitahidi
kufuata masharti na nafuu naiona isipokuwa suala la maji nashindwa maana
ninapokunywa ‘gambe’, mpaka muda wa kuniamsha kunywa dawa nakuwa
sijanywa maji na daktari aliniambia nisipofanya hivyo naweza kupata
kansa,” alisema Kajala.
CHANZO: GPL
Post a Comment