Mpenzi Mpya wa Nuh Mziwanda naye ajichora tattoo ya Nuh
Mpenzi mpya wa Nuh Mziwanda akioneshea picha ya tattoo inayoonesha jina la staa huyo.
Tattoo aliyekuwa amechora mpenzi wa Nuh wa kwanza, Shilole ambaye baadaye walipoachana alikuja kuifuta.
Mpenzi mpya wa Nuh Mziwanda ambaye jina lake halijawekwa wazi naye amejichora tattoo yenye jina la Nuh Mziwanda.
Kupitia ukurasa wa Nuh wa Instagram, Nuh
ambaye aliachana na Shilole kabla hajampata mpenzi wake huyo alitupia
picha ikimuonesha akiwa amekumbatiwa na mpenzi wake huyo mpya huku
tattoo yenye jina la staa huyo ikianikwa kisha akaandika;
“Asante mchumba wangu wa kweli wa shida na raha.”
Awali Nuh alikuwa akitoka na Shilole mpaka
hatua ya kufikia kuandikana tatooo ambapo shilole alimuandika Nuh tatoo
ya kifuani na mkononi na Nuh naye akajichora ya Shilole mkononi. Kwa
sasa wawili hao walishafuta tatoo zao.
CREDIT: Andrew Carlos/GPL

Post a Comment