Quick Rocka: Penzi la Kajala halinitesi
Quick Rocka na Kajala Masanja.
MSANII anayekimbiza katika
Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, Quick Rocka amedai kuwa penzi la muuza
sura kwenye Filamu za Kibongo, Kajala Masanja halimtesi maana ni la
kishkaji na kila mmoja kati yao ana uhuru wa kufanya mambo yake binafsi
kutokana na matakwa yake bila kumbana mwenziye.
Akipiga stori na safu hii ya burudani
Quick ambaye kwa sasa ameachia ngoma mpya iitwayo Hapo aliyomshirikisha G
Nako alisema, tofauti na watu wengi waliyoko kwenye mapenzi wanaokuwa
wanabanwa na wapenzi wao katika shughuli za kawaida kwa ajili ya
kujitafutia kipato, kwake haiko hivyo, yeye na Kajala wamepeana uhuru.
“Sijui nikweleze vipi kuhusu penzi langu
na huyo diva, wewe elewa tu liko kishkaji, kila mtu ana uhuru wa
kufanya mambo yake na haina kubanana, hata hivyo wakati mwingi ninakuwa
naye,” alisema Quick Rocka.
Alipoulizwa juu ya tetesi zinazosambaa
za Kajala kutoka na msanii wa Bongo Fleva, Msami alisema hajui chochote
kuhusu wawili hao.

Post a Comment