WATOTO 2.7 WAMEDUMAA KUTOKANA KUKOSA LISHE BORA –PANITA
Mkurugenzi
wa Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita), Tumaini Mikindo akizungumza na
viongozi wa dini jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Lishe nchini.
Mchungaji
wa makanisa ya Kipentekoste, Sixtus Mallya akichangia mada hasa kwenye
imani za dini kukataza baadhi ya vyakula na kusema kuwa vyakula hivyo
vimekatazwa na Biblia amesema kuwa lishe ni kitu cha mhimu kwa ukuaji wa
mwili.
Baadhi ya Vyakula Lishe ambavyo vinatakiwa kwa kila mlo ambavyo vinatakiwa kila mtu anapokula.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WATOTO
milioni 2.7 sawa na asilimia 35 wana udumavu kutokana na kukosa
lishe hali inayofanya serikali kupoteza pato la taifa katika kuhudumia
watoto hao.
Utadumavu huo umepungua kutoka asilimia 42 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 35 mwaka 2015.
Akizungumza
katika mkutano wa viongozi wa dini katika suala lishe, Mkurugenzi wa
Jukwaa la Lishe Tanzania (Panita), Tumaini Mikindo amesema viongozi wa
dini wana umuhimu kuwa mabalozi wa kuhamasisha lishe katika ngazi ya
familia katika nyumba za ibada.
Amesema
kuwa kiwango cha watoto waliodumaa hawawezi kurekebishika kutokana na
kuadhiri maumbile ya mtoto pamoja na kinga yake kuwa duni kwa ugonjwa
wa utapiamlo.
Mikindo
amesema kuwa suala la lishe haliangaliwi huku likiwa linaadhiri
maendeleo ya familia kutokana na malezi ya mtoto aliyedumaa ni tofauti
na mtoto asiyedumaa.
Nae
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Pazi Mwinyumvua amesema kuwa
wanawake wanashindwa kunyonyesha watoto kwa sababu kulinda maumbile
kwani mwanamke akinyonyesha kuwa maziwa yanaanguka.
Mwinyimvua amesema wanashindwa kula chakula na mbogamboga kwa madai kula mboga mboga ni suala la watu wenye kipato cha chini.
Post a Comment