UKAWA Wanawake walivyotoka Nje ya Bungeni kisa kuitwa ‘Baby’
Umoja wa Wabunge wanawake UKAWA wametoka nje ya ukumbi wa Bunge Dodoma baada ya jana Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga kusema kuwa ‘Wabunge wote wa viti maalum CHADEMA ili wapate nafasi hizo ni lazima waitwe kwanza Baby‘
Kauli iliyopingwa na baadhi ya wabunge na kumtaka Naibu Spika kutumia kiti chake ili Mlinga
atengue kauli yake, Mlinga alikubali kuitengua lakini Leo Mei 06 2106
hoja hiyo ikarejeshwa tena bungeni kuwa ni kauli ya udhalilishaji kwa
wanawake.
Mbunge wa Kawe Halima Mdee amezungumza nje ya Bunge na kusema..>> ‘Jana
mbunge Goodluck Mlinga wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Katiba na
Sheria alisema Wabunge wote wa viti maalum Chadema ili apate nafasi za
kuwa Wabunge ni lazima awe Baby wa mtu‘
‘Sisi
ni wajumbe wa umoja wa wanawake, tunajua nchi hii ina mfumo dume,
lakini jana wakati wabunge wanawake wanadhalilishwa kuna wabunge
wanawake haohao walikuwa wanapiga makofi ‘
‘Tumewaambia
viongozi wetu na tumekubaliana kama wabunge wote kuwa tunaenda kuandika
barua kujitoa kwenye chama cha Wabunge Wanawake‘
Wabunge wanawake wakiwa wamesimama kupinga
.

Post a Comment