KLABU ZAPEWA 'CHUMBA' KUTOA MAONI KUHUSIANA NA UBORESHAJI WA LIGI...
Bodi
ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka (TFF) imezipongeza timu za Ligi Kuu
Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya msimu wa Ligi Kuu Bara kuwa ya
Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio.
Bodi
hiyo imezifahamisha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa
2016/17 kuwa mchakato wa wa utengenezaji kanuni umeanza.
Bodi
ya Ligi kwa sasa inakaribisha maoni, mapendekezo, marekebisho kutoka
klabu ili kuboresha uendeshaji wa ligi. Maoni hayo yanapokelewa kwa njia
ya maandishi moja kwa moja kwenye ofisi za bodi au kwa njia ya barua
pepe tplb.tplb@yahoo.com

Post a Comment