WAAMUZI WA GHANA, ETHIOPIA KUICHEZESHA YANGA DHIDI YA WAANGOLA
Mwamuzi
Joseph Odartei Lamptey, Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa
kati katika mchezo wa kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani
Afrika utakaozikutanisha timu za Young Africans ya Dar es Salaam,
Tanzania na GD Sagrada Esperanca ya Angola.
Lamptey
kutoka jiji la Accra, Ghana atasaidiwa na raia wenzake wa nchi hiyo
kuchezesha mchezo huo Na. 99. Mwamuzi Msaidizi Na. 1 (line 1) ni David
Laryea wakati Mwamuzi Msaidizi Na. 2 (line 2) ni Malik Alidu Salifu.
Mwamuzi
Msaidizi mezani (Fourth Official) ni Cecil Amately Fleischer huku
Kamishna wa mchezo huo, akiwa ni Asfaw Luleseged Begashaw wa Ethiopia.
Viingilio
na upatikanaji wa tiketi utatangazwa kesho Ijumaa Mei 6, 2016 na
uongozi wa klabu ya Young African mara baada ya mkutano kati ya makocha
wa timu zote mbili. Mkutano wa makocha hao utafanyika saa 5.00 mchana
kwenye Ukumbi wa mikutano wa TFF.

Post a Comment