Rais Magufuli Amjulia Hali Mufti Mkuu Wa Tanzania Pamoja Na Kufanya Ukaguzi Wa Kushtukiza Katika Wodi Ya Wazazi Ya Hospitali Ya Taifa Ya Muhimbili
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea
kwa ghafla wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini
Dar es salaam, na kujionea hali ya msongamano mkubwa wa wazazi
uliosababishwa na uhaba wa vitanda na nafasi finyu katika wodi hiyo.
Rais Magufuli aliyekuwa akitoka katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokwenda kumuona na kumjulia hali Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubery Bin Ally, amelazimika kwenda katika wodi hiyo baada ya msafara wake kusimamishwa na kundi la akina mama, waliomtaka kwenda katika wodi ya wazazi ili akajionee jinsi wazazi wanavyokabiliwa na kero mbalimbali ikiwemo ya kulala chini kutokana na kukosa vitanda.
Baada ya kujionea mwenyewe kero ya msongamano na kuzungumza baadhi wazazi waliojifungua, Rais Magufuli amewaahidi wazazi hao kuwa atashughulikia kero alizozishuhudia.
"Nimeiona hali halisi mimi mwenyewe, watu wanapata shida, watu wana mateso, na ndio maana nimeamua kuja kwa makusudi, sikuomba ruhusa ili nijionee hali ilivyo, nimejifunza mengi, ninayabeba na nitajua namna ya kuyatatua" Alisema Rais Magufuli.
Kabla ya kutembelea wodi ya wazazi, Dkt. Magufuli amemjulia hali Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubery Ally aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo amempa pole na kumuombea apone haraka.
Pamoja na kupokea pole ya Rais, Mufti wa Tanzania ameongoza dua ya kumuombea heri Rais Magufuli ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake katika kuwahudumia watanzania.
Dua kama hiyo pia imefanywa na wananchi wengine waliokuwa wakimsubiri nje ya majengo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo katika dua hiyo wamemuomba Mwenyezi Mungu kumlinda na kumuongoza katika majukumu yake ya kuiongoza nchi.
"Mwenyezi Mungu mbariki Rais wetu, mpe hekima, busara na upendo katika kazi zake za kuiongoza nchi hii ili watanzania wote wanufaike" ilisema sehemu ya dua hiyo iliyoongozwa na mmoja wa akina Mama.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
10 Februari, 2016.

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia
hali Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir ambaye
amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Mufti
na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akimuombea Dua
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara
baada ya Rais Dkt. Magufuli kumjulia hali Hospitalini hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa
Dua na ndugu na jamaa mbalimbali ambao walifika Muhimbili kuwaona
wagonjwa wao.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea
katika Wodi ya Wazazi kufanya ukaguzi wa ghafla mara baada ya kuwasili
akitokea Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya Wazazi na amewahidi kutatua kero
zao ndani ya muda mfupi ujao.PICHA NA IKULU

Post a Comment