Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Aiangukia Serikali Kuomba Msaada Baada ya Wananchi Kuvamia Shamba Lake La Ekari 33
WAZIRI
Mkuu Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye, ameiangukia serikali na kuomba
msaada baada ya wananchi kuchukua sheria mkononi na kuvamia eneo lake la
ekari 33 lililopo Mabwepande katika Manispaa ya Kinondoni nje kidogo ya
jiji la Dar es Salaam.
Serikali
imemuahikikishia Mhe. Sumaye kuwa haina mpango wa kumkandamiza mtu
mnyonge wala tajiri hivyo itahakikiha inatoa haki kwa kila mmoja baada
ya wiki mbili kwa kua imesikiliza pande zote mbili katika mgogoro huo.
Akizungumza
katika kikao cha pamoja kati ya wananchi wa kitongoji cha Kimondo mtaa
wa mji mpya Kata ya Mabwepande na Mhe. Sumaye Dar es Salaam jana
asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alisema ili kumaliza
mgogoro huo ambao Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye ameiomba serikali
kuingilia kati ni lazima busara kutumika.
Alizitaka
pande hizo mbili kuiachia serikali kwa wiki mbili ili kutafuta njia
bora ya kumaliza tatizo hilo huku wananchi wakitakiwa kuacha kuendelea
na ujenzi na kugawiana maeneo katika shamba hilo.
“Serikali
ya Rais Magufuli ni sikivu na ndio maana ilikuwa tayari kumsikiliza
Waziri Mkuu wetu Mstaafu Sumaye na kusikiliza wananchi. ili kutenda haki
tunatambua migogoro ya ardhi ilivyokuwa na athari kwa jamii hatuna
mpango wa kumkandamiza tajiri wala mnyonge,”alisema.
Alisema
katika eneo hilo anajua jinsi wananchi walivyotumia nguvu katika
kuwekeza ujenzi na rasilimali zao lakini kwa sasa wasitishe shughuli
hizo na kuendelea kugawana maeneo na Sumaye pia kuacha uwekezaji ili
kutafuta suluhu.
"Zipo
njia nyingi tutazitumia kumaliza mgogoro huu ikiwemo kufuata sheria kwa
kuangalia iwapo mzee wetu alikiuka taratibu za kumiliki ardhi kama
ilivyodaiwa na wananchi ili tujue hatua za kuchukua,”alisema.
Alisema
pia wanaweza kukaa na Sumaye na kuzungumza naye ili kukubali hasara kwa
kutoa eneo kidogo na kuwapatia wananchi hao ambao hawana makazi au
Manispaa kutafuta eneo mbadala na kuwauzia kwa bei nafuu.
Alizitaka
pande hizo mbili kutambua umuhimu wa kulinda amani katika mgogoro huo
kwa changamoto zilizopo kutatuliwa bila kutumia nguvu.
Makonda pia aliagiza serikali ya kijiji kufanya utambuzi wa wananchi hao wenye makazi katika shamba la Sumaye.
Awali
katika mkutano huo Mhe. Sumaye alimueleza Mhe. Makonda jinsi serikali
ilivyo na kazi ngumu ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kuomba
kutumia busara zake kumpatia eneo hilo analomiliki kihalali.
“Mheshimiwa
Mkuu wa Wilaya kama nilivyokueleza awali serikali yetu inakazi ngumu
sana hasa kutokana na viongozi wa chini kutokuwa wasikivu na wakweli
.Eneo hili namiliki kihalali ,nina nyaraka zote na ninalipia kila mwaka
na nilikuwa katika mpango wa kutafuta wafadhili ili kuliendeleza kwa
kujenga Chuo Kikuu,”alisema.
Alisema yeye na familia yake waliuziwa eneo hilo toka mwaka 1997 na anaamini serikali itatenda haki.
Diwani
wa kata hiyo Suzan Masawe alisema anauthibitisho kuwa eneo hilo
lilikuwa pori na Sumaye alilitelekeza kwa muda mrefu na kusababisha
uhalifu ikiwemo wanawake kubakwa,mali za wizi kufichwa na uhalifu
mbalimbali.
Alisema
kutokana na hatua hiyo walimtafuta Sumaye lakini hakuwa na
ushirikiano kwakuwa hata alipofanya uwekezaji kwa kuchimba kisima cha
maji alikataa kuwapa wananchi .
Suzan
alisema kutokana na hasira za wananchi hao kwa kukosa huduma za kijamii
kwa muda mrefu ikiwemo eneo hilo kutokuwa na shule,Zahanati wala kituo
cha polisi waliamua kuvamia na kujigawia maeneo.
Mmoja
wa wananchi hao Athuman Mnubi alikiri kweli hawana umiliki halali wa
eneo hilo na katika hatua ya kutafuta makazi walivamia msitu huo
uliotelekezwa na Sumaye.
Alisema
wanaamini kutokana na ahadi ya serikali ya Rais Magufuli katika kupora
maeneo yaliyotelekezwa na wawekezaji watasaidiwa.
WAKATI
huo huo Makonda alisimamisha na kukamata baadhi ya malori ya kokoto na
mchanga, wafanyakazi na Mwekezaji wa kigeni kutoka India Sules Waljan
wanaochimba mchanga,kokoto na kifusi katika eneo la Mabwepande.
Hatua
hiyo imekuja baada ya kuona uharibifu mkubwa wa mazingira na
alipowahoji wafanyakazi na Mwekezaji huyo kama wanavibali walisema
hawana.
Makonda
amewafikisha watuhumiwa hao kituo cha polisi cha Wazo Hill ili kutoa
maelezo ya kina na kusema kuwa serikali inatumia gharama kubwa kwa
uhalibifu huo wa mazingira ambao pia unafanywa katika vyanzo vya maji na
matengenezo ya madaraja yanayoharibiwa ni makubwa.
Hapa Sumaye na viongozi wengine wakitafakari jambo.
DC Makonda akihutubia katika mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mabwepande, Suzan Masawe.
Mheshimiwa Sumaye (kushoto), akiongoza kuonesha mpaka wa shamba lake.
Mhe. Sumaye akielezea uhalali wake wa kumiliki eneo hilo.





Post a Comment