Wabunge wa upinzani watoka tena bungeni leo

Hali ya sintofahamu imeendelea kugubika vikao vya bunge
vinavyoendelea mjini Dodoma baada ya wabunge wote wa upinzani leo kutoka
nje ya bunge mara baada ya wabunge kuanza kuchangia hotuba ya rais.
Baada
ya kipindi cha maswali na majibu, yalifuata matangazo na baada ya hapo
wabunge walitakiwa kuanza kuchangia hotuba ya Rais Magufuli lakini
baadhi ya wabunge wa upinzani walianza kuomba mwongozo kuhusu kauli ya
waziri mkuu kuhusu ishu ya michango ya chakula wanayoendelea kulipishwa
wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule za bweni.
Hata hivyo, licha ya baadhi ya wabunge wa Ukawa akiwemo Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea kuendelea kuomba mwongozo, naibu spika aliwanyima nafasi hiyo, jambo lililosababisha wasusie kikao hicho na kutoka nje huku wakilalamika kwamba wamezibwa midomo.

Post a Comment