YANGA YAFIKIA UAMUZI WA KUACHANA NA MBRAZIL COUTINHO
Kiungo Andrey Coutinho yuko jijini Dar es
Salaam, lakini uongozi wa Yanga, umepitisha uamuzi wa kumtema.
Habari zinaeleza Yanga iko katika hatua za
kufikia makubaliano na
Coutinho ili kuvunja mkataba wake.
Kocha Hans van der Pluijm ameridhia kuachana na
Coutinho kwa
kuwa amekuwa hana msaada wa kutosha.
Lakini Yanga kwa sasa inafanya mchakato huo, kama pande mbili zitashindwa kufikia mwafaka, basi raia huyo wa Brazil ataendelea kubaki Yanga hadi mkataba wake utakapokwisha.
Post a Comment