Rais Magufuli amuweka njia panda Chiza
Rais
John Magufuli ameshangazwa na kauli ya Mwenyekiti wa bodi ya
Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara nchini Christopher Chiza
kuwa na mipango ya kujenga majengo mapya kwa ajili ya wafanyabiashara
badala ya viwanda vitakasaidia nchi.
Akizungumza
leo wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa,
Rais Magufuli amesema kwamba ameshangazwa sana na mipangio ya kujenga
mahoteli pamoja na kufanyia ukarabati wa majengo kwani hajui mahali pesa
hizo zitakapopatikana.
"Mh.
Chiza amezungumza kubadilisha majengo na kujenga mapya, mawazo mazuri
lakini najiuliza hizo hela zimetoka wapi , haingii akilini wao ndio
wanatusisitizia mambo ya biashara na viwanda na 'theme' ya mwaka huu
inazungumzia kukuza biashara na maendeleo ya viwanda sasa wao badala ya
kuzungumza juu ya maendeleo ya viwanda wanataka wajenge Hotel hapa,
watengeneze majengo mapya sasa. Sijaelewa, sasa kama hizo hela zipo basi
mzipeleke mkajenge kiwanda cha mfano
Aidha
Rais magufuli amesisitiza kwamba "Haya majengo yaliyopo ambayo
mnayaona yamechakaa hawa wanaokuja kuonesha bidhaa zao wapeni bure
wajenge ili kila mwaka wawe wanaonesha, hiyo Hoteli kwani mkijenga
lazima walale hapa hapa? Mnaweza kujenga hoteli hapa bado wakaenda
mjini. Mimi nilifikiri badala ya kujenga jenga majengo fikirieni zaidi
katika kujenga viwanda kwa ajili ya mfano wa kuonesha Wizara kweli iko
mbele kwa ujenzi wa viwanda.
Katika
kuonyesha nia ya kufikia Tanzania ya viwanda inafikiwa Rais ameitaka
wizara pamoja na bodi hiyo kutofikiria ujenzi wa majengo.
"Mwenyekiti
nimekuteua juzi umeshaanza kufikiria majengo hapa pamoja na Bodi yako
mnanifanya nifikirie zaidi. Haya majumba yanaweza yakawa siyo mazuri
sana lakini ni mazuri kwa watu wa Tanzania ambao wanataka kuona bidhaa.
Yanayowaleta hapa siyo majumba Watanzania wanakuja hapa kuangalia
Teknolojia na vifaa vilivyomo.Inawezekana mimi nipo tofauti mnisamahee
lakini katika muelekeo wangu ninaona hizo hela mnataka kuzitumia vibaya"
Rais alisisitiza.
Pamoja
na hayo Mh. Rais amewaomba waandaji wa maonyesho hayo pamoja na Waziri
wa viwanda na biashara Mh. Charles Mwijage kuongeza siku zaidi katika
maonesho ili watanzania waweze kupata muda mzuri wa kununua na
wafanyabiasha kuuza ambapo ombi lake lilikubaliwa hapo hapo na kuongezwa
siku tano mbele.
Post a Comment