Wolper akivishwa pete tu kwisha habari yake!
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper.
KUMBE! Waliosema ujana maji ya moto
hawakukosea kwani una changamoto nyingi hasa pale unapofikia wakati wa
kumtafuta wa kuwa naye maishani yaani mke au mume.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline
Wolper Massawe anaweza kuthibitisha hilo baada ya uchunguzi kuonesha
kuwa ana listi ya wanaume waliomvisha pete za uchumba kisha wakapata
walichokitaka, wakaingia mitini.
Uchunguzi huo ulibaini kwamba, wanaume wengi wamekuwa wakitumia gia hiyo kumrubuni na kumwachia maumivu makali ya moyo.
Katika makala haya tunakuletea listi ya
wanaume ambao waliwahi kuwa na Wolper na kumvisha pete za uchumba na
wengine kujitambulisha au kumtambulisha kabisa kwa wazazi lakini baada
ya kumfaidi wakammwaga na kujikuta akihamia kwa mwingine, jambo ambalo
watu wengine ambao ni mashabiki wake wamekuwa wakihoji ana nini mpaka
yamkute hayo?
ABDALLAH MTORO ‘DALLAS’
Mfanyabiashara huyo aliyekuwa na fedha ‘chafu’ alianzisha uhusiano na Wolper ambapo alimvisha pete ya uchumba na kumtambulisha mpaka kwa wazazi wake naye kujitambulisha kwa wazazi wa mwanadada huyo lakini walimwagana baada ya Wolper kuhisi kwamba anasalitiwa kwa mpenzi wake huyo kuwa na uhusiano na wasanii wenzake.

Dallas alikuwa akimpa Wolper fedha za
kutosha ambapo kipindi hicho aliweza kumchangia msanii mwenzake ambaye
ni marehemu kwa sasa, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kiasi cha Sh. milioni 15
kwa ajili ya matibabu nchini India huku katika kumbi mbalimbali za
starehe akitunza kama hana akili nzuri.
Jamaa huyo ni mfanyabiashara anayemiliki maduka ya viatu na nguo maeneo ya Kinondoni jijini Dar ambapo baada ya Wolper kuachana na Dallas naye aliingia kwa gia ya kumvisha pete ya uchumba na mapenzi kuwa motomoto kwa kile kilichoonekana kwamba anampooza machungu.
Hawakukaa muda mrefu, wawili hao
waliachana japokuwa sababu za kumwagana kwao hazikujulikana ila tayari
jamaa huyo alikuwa ameshamfaidi Wolper.
JIMMY MGAYA
Jimmy ni Mbongo aishiye Afrika Kusini ‘Sauz’ ambaye naye ni mfanyabiashara pia. Baada ya Wolper kuachana na Gee Modo alinasa kwa Jimmy ambapo kwa mara ya kwanza zilinaswa picha zao za kimahaba wakiwa nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kudaiwa
kuvishwa pete ya uchumba, kama ilivyokuwa kwa wengine, uhusiano huo
haukudumu kwa muda mrefu ukavunjika.
MWAMI RAJABU
Mwami ni mfanyabiashara wa madini ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mara nyingi Mwami hupatikana jijini Dar kwa kazi zake za kibiashara ambapo hufikia hoteli za kifahari.
Mwami ni mfanyabiashara wa madini ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mara nyingi Mwami hupatikana jijini Dar kwa kazi zake za kibiashara ambapo hufikia hoteli za kifahari.
Mwami anatajwa kwamba aliwahi kumvisha
pete ya uchumba Wolper lakini hakuna kilichoendelea baada ya jamaa huyo
kudaiwa kupata alichokitaka.
Wolper na Mwami walianzisha uhusiano
ambapo mwanadada huyo alikuwa na fedha za kumwaga lakini waliachana huku
sababu zikiwa hazijulikani, japokuwa mfanyabiashara huyo anadaiwa kuwa
na uhusiano na mastaa mbalimbali wa Bongo baada ya kuachana na Wolper.
MKONGO
Katika kujaribu tena bahati yake, Wolper aliingia kwa Mkongo mmoja ambaye mpaka wanaachana jina lake halikupatikana. Kama ilivyokuwa kwa wengine, uhusiano huu haukuchukua muda mrefu na kuvunjika.
Katika kujaribu tena bahati yake, Wolper aliingia kwa Mkongo mmoja ambaye mpaka wanaachana jina lake halikupatikana. Kama ilivyokuwa kwa wengine, uhusiano huu haukuchukua muda mrefu na kuvunjika.
Mkongo huyo alimvisha Wolper pete ya
uchumba na alikuwa akisema mara kwa mara kuwa wapo kwenye mipango ya
ndoa hata pale ukweli ulipogundulika kwamba ni mume wa mtu ambapo Wolper
alidai atakomaa mpaka mwisho wa siku wakaja kumwagana baada ya Mkongo
kumfaidi mrembo huyo.
CHANZO: GPL
Post a Comment