JB abainisha kinachoiua sanaa!
Mkongwe wa filamu Bongo, Jacob Stephen ‘JB’.
MKONGWE wa filamu Bongo, Jacob
Stephen ‘JB’ ameweka wazi kinachochangia sanaa ya filamu ionekane kama
imepwaya na kukosa thamani katika soko kuwa ni wasanii kuishiwa ubunifu
na mipango mikakati ya kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
Akichonga na kona ya Bongo Movies, JB
alisema kuwa sanaa kama sanaa ipo na kamwe haiwezi kufa, isipokuwa
vizazi ndani ya sanaa ndiyo hubadilika kulingana na nyakati, lakini mtu
yeyote anaweza kuja na kitu kipya kinachogusa maisha ya kawaida na
kuwika, kuliko hata waigizaji wakongwe.
“Kwani muziki wa Kongo si ulionekana
kama umekufa, lakini baada ya Koffi Olomide kuachia Ngoma ya Selfie,
muziki wao haujarejesha heshima yake? Kwa hiyo sanaa huwa haifi ila watu
ndiyo huishiwa.
Post a Comment