ad

ad

Undani kigogo bandari kufa kwa presha!

2-001Elia Eliampenda Kimaro.
Chande Abdallah na Deogratius Mongela
WAKATI Rais John Magufuli akiwa kwenye zoezi la kutumbua majipu kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), mshtuko mkubwa umetokea kufuatia kigogo mwenye wadhifa wa Artsan One (TPA) jijini Dar, Elia Eliampenda Kimaro (51) kufariki dunia ghafla kwa shinikizo la damu (presha) akiwa nyumbani kwake, Mikwambe, Kigamboni, Dar.
KIGOGO BANDARI (4)-001Kwa mujibu wa chanzo chetu, Kimaro alifariki dunia Novemba 30, mwaka huu kwa uthibitisho wa daktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako marehemu alikimbizwa kwa ajili ya matibabu.
WAKATI MBAYA
Kifo cha Kimaro kimetokea wakati kukiwa na sintofahamu kubwa miongoni mwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuhusiana na utolewaji wa makontena 349 kinyemela na kuisababishia serikali kukosa mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 80.
KIGOGO BANDARI (5)-001KWA MUJIBU WA FAMILIA
Taarifa kutoka ndani ya familia, marehemu alisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu. Lakini ghafla alfajiri ya Novemba 30, hali yake ilibadilika na hivyo kukimbizwa Muhimbili ambako daktari alisema alishafariki dunia.
WAOMBOLEZAJI WAKUBWA
Risasi Jumamosi ambalo liliweza kufika msibani, liliwashuhudia wafanyakazi wengi wa bandarini na TRA bandarini wakiwa hapo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
KIGOGO BANDARI (6)-001YALIYOSEMWA MSIBANI
Baadhi ya wafanyakazi hao, walisikika wakidai, marehemu alikuwa miongoni mwa vigogo waliokuwa wakichunguzwa kwa utolewaji wa makontena 349 siku chache zilizopita.
“Pia nasikia baada ya waziri mkuu (Kassim Majaliwa) kutoa mwongozo siku zile bandarini, watu wa usalama wa taifa walishamfuata hapa kwake mara kadhaa na kumhoji.
KIGOGO BANDARI (3)-001Lakini pia, kuna madai kwamba, miamala yake ya kibenki nayo ilifuatiliwa na jamaa hao ambapo walikuta pesa nyingi,” alisikika akisema mmoja wa wafanyakazi hao ambaye alipogundua kuna mapaparazi wetu, alifunga kinywa.
UTAJIRI WAKE WAZUNGUMZIWA
Nao baadhi ya waendesha bodaboda wa eneo hilo, walionekana kushangazwa sana kufuatia taarifa za kifo cha kigogo huyo, wakidai siku moja kabla, walionana naye akiwa mzima wa afya.
KIGOGO BANDARI (1)-001Hata hivyo, walisema mara baada ya taarifa za kifo, walishangaa kuona magari yake ya kifahari yakiondolewa kutoka nyumbani kwake hapo:
“Labda waliyapeleka mahali ili kupata nafasi ya kuweka maturubai ya msiba. Si unajua majumba haya ya ghorofa, yana nafasi zaidi ya kwenda juu kuliko upana,” alisema mmoja wa bodaboda hao.
Mwendesha bodaboda mmoja alisema: “Mzee wa bandari alikuwa mtu poa sana. Hata madereva wa daladala zake wameumia. Unajua jamaa alikuwa na mkwanja wa maana. Hii nyumba ya hapa ‘cha mtoto’, ana nyumba nyingine Yombo (Dar), magari ndiyo usiseme. Yaani tumempoteza mtu muhimu sana.”
KIGOGO BANDARI (2)-001TUKIO LA AJABU
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanaume mmoja aliyesema yeye ni ndugu wa marehemu, alipombaini mpigapicha wetu, alimtimua huku akikataa kuongea chochote kuhusu marehemu huyo, akasema: “Wapigapicha wa tukio hili walishakodishwa na familia na wanajulikana. Hivyo waandishi wa habari hawatakiwi hapa.”
MAZISHI
Marehemu Kimaro alizikwa Desemba 2, mwaka huu kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar. Ameacha mke na watoto wanne.
CHANZO: GPL
Powered by Blogger.