Ummy Mwalimu: Wakuu wa mikoa hakikisheni mnapambana na kipindupindu
WAZIRI wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza wakuu wa mikoa, wilaya
na kata kuhakikisha wanakuwa na kikosi kazi cha kupambana na kipindupindu na
kutoa ripoti ya utekelezaji kwa ngazi za juu kila siku.
Akizungumza na wanahabari
leo jijini Dar es Salaam akiwa makao makuu ya wizara yake, Mwalimu, amesema pamoja na kuwa na kuwa na vikosi
vinavyoshughulikia masuala ya afya lakini, viongozi na watendaji wa mikoa na
halmashauri wasimamie majukumu yao ya kukagua na kusimamia usafi katika kila
kaya na kila siku ili kuboresha hali ya usafi na kuchukua hatua za kisheria kwa
wanaokiuka.
Mwalimu amesema shule
zote pamoja na vyuo na taasisi zinazoendelea kutoa mafunzo zizingatie kanuni za
afya ili kuzuia ugonjwa usiingie na kuenea katika maeneo yao.
Aidha aliwataja watu 11,257 waliopata ugonjwa huo tangu
ugonjwa huo ulipoanza na kati yao jumla
ya watu 177 wameshafariki kwa ugonjwa huu ambao ni sawa na asilimia 1.5 ya waliougua.
Aidha, Waziri Mwalimu
alitaja mikoa ambayo imekuwa na wagonjwa wengi tangu mlipuko uanze kuwa ni Dar
es Salaam watu 4,628 ambayo ni asilimia 41 ya wagonjwa wote, ikifuatiwa na Tanga watu 1443 ambayo ni asilimia
13, Singida watu 955 ambayo ni asilimia 8,
Mwanza watu 841 ambayo ni 7 asilimia.
Katika mazungumzo hayo,
waziri huyo amepiga marufuku uuzaji wa matunda yaliyomenywa na chakula katika
maeneo ya wazi kutokana na kuibuka kwa kasi ya ugonjwa huo.
Pia amewaagiza maafisa
afya kuhakikisha wauzaji wote wa vyakula wanazingatia kanuni za usafi ikiwa ni
pamoja na kuosha vyombo kwa kutumia sabuni na kwa maji salama ya moto na sabuni.
1.Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto)akisoma
taarifa yake na kulia kwake ni Naibu Waziri, Dk. Hamis Kigwangala anayesaidiana
naye wizarani hapo, wakizungumza na wanahabari.
NA DENIS MTIMA/GPL
Post a Comment