November 30 2015 ilikuwa ni siku ambayo FIFA walitangaza majina ya wachezaji soka watatu waliofanikiwa kuingia katika fainali ya kuwania tuzo ya Ballon d’Or
2015, pamoja na kutaja magoli matatu bora yanayowania tuzo ya goli bora
la mwaka na majina matatu ya wanaowania tuzo ya kocha bora wa mwaka.
Ukumbi ambao zimetolewa tuzo za LALIGA za msimu wa 2014/2015
Kama ulikuwa hujui mtu wangu wa nguvu usiku wa November 30 kuamkia December 1 ilikuwa ni siku ya utoaji wa tuzo za Ligi Kuu Hispania LALIGA kwa wachezaji na makocha waliofanya vizuri katika msimu wa mwaka 2014/2015, tuzo ambazo zilitolewa katika jiji la FC Barcelona, baadhi ya majina ya wachezaji waliofanikiwa kutwaa tuzo hizo ni Lionel Messi, Neymar, Sergio Ramos, James Rodriguez na kocha bora akitajwa kuwa Luis Enrique wa FC Barcelona.
Baadhi ya watu waliohudhuria tuzo hizo
Diego Simeone kocha wa Atletico Madrid ni miongo mwa watu waliohudhuria wa pili kutoka kushoto.
Wadau wa soka katika Red Carpet dakika chache kabla ya utolewaji wa tuzo haujaanza.
Sergio Ramos na shabiki
Red Carpet wadau katika picha ya pamoja
Neymar akiwasili ukumbini na kupiga picha kabla ya utolewaji wa tuzo kuanza
Golikipa wa FC Barcelona Claudio Bravo
Lionel Messi akiwasili ukumbini
Kocha wa FC Barcelona Luis Enrique ndio aliibuka mshindi wa tuzo ya kocha bora
Aliyekuwa kiungo wa FC Barcelona Xavi Hernandes alitajwa kuwa kiungo bora.
Claudio Bravo wa FC Barcelona alitangazwa kuwa golikipa bora wa msimu
Beki bora alikuwa ni Sergio Ramos wa Real Madrid
Neymar alitwaa tuzo ya mchezaji bora kutoka bara la America
James Rodriguez wa Real Madrid alitangazwa kuwa kiungo bora wa msimu
Claudio Bravo akiwa na tuzo yake ya golikipa bora
Lionel
Messi akiwa na tuzo yake ya mchezaji bora wa msimu wa 2014/2015 lakini
ameshinda tuzo mbili na mshambuliaji bora wa msimu huo.
Baadhi ya washindi katika picha ya pamoja
Post a Comment