ADEBAYOR AAMUA KUSAFIRI KUREJEA ENGLAND, SAFARI HII NI CHELSEA AU WATFORD
Chelsea na Watford ndiyo
klabu mbili zitakazomrudisha mshambuliaji Emmanuel Adebayor nchini England.
Adebayor ameamua
kusafiri kwenda England tena wiki ijayo na imeelezwa kuna uhakika atafanya
mazungumzo na kati ya klabu hizo mbili, moja wapo anaweza kujiunga nayo kwa
ajili ya Ligi Kuu England.
Hiyo ni baada ya wiki
kadhaa za kuvunja kwake mkataba na klabu yake ya Tottenham na baada ya hapo
aliamua kurejea kwao Togo na kuendelea na maisha.
Lakini sasa, anarejea
kwa kuwa karibu dirisha la usajili linafunguliwa.
Msimu uliopita
aliichezea Spurs mechi 17 na kufunga mabao mawili tu. Mechi yake ya mwisho
aliichezea Spurs alipoanza lakini akatolewa wakati walipopata kipigo cha bao
1-0 kutoka kwa Man City.
Mechi yake ya mwisho ya
mashindano kufunga bao ilikuwa ni Oktoba 2014 wakati Spurs ilipoivaa Newcastle.
Post a Comment