Azma ya kuwa na kizazi kisicho na UKIMWI, muda wa vitendo ni sasa
Na Mark B. Childress, Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mwaka
mmoja uliopita wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani,
niliandika makala kuhusu jitihada za kuwa na kizazi kisicho na UKIMWI
nchini Tanzania. Toka wakati huo, kwa pamoja tumepiga hatua muhimu
kuelekea katika kufikia azma hiyo, tukielekeza rasilimali na shughuli
zetu kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi nchini kote. Hata hivyo, bado
tunahitajika kuongeza nguvu na kufanya zaidi. Bila ya kuongeza kasi yetu
katika mwelekeo huu, maambukizi mapya yataongezeka, jambo
litakaloongeza idadi ya Watanzania watakaokuwa wakiishi na VVU hivyo
kuathiri maendeleo na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Post a Comment