Nape Akaribishwa Ofisi za Wizara Yake
Waziri wa Wizara wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akizungumza mbele ya wafanyakazi wa wizara hiyo.
Waziri wa Wizara wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akizungumza mbele ya wafanyakazi wa wizara hiyo.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye, leo amekaribishwa na wafanyakazi wa wizara yake kwenye ofisi zao baada ya kuchaguliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa waziri wa wizara hiyo.
Nape amehudhuria hafla fupi ya kumkaribisha hii ofisi za Wizara hiyo zilizopo katika Jengo la Golden Jubilee jijini Dar es Salaam, ambapo kwenye hafla hiyo amesema kuwa wafanyakazi wa chini hadi ngazi za juu wanatakiwa kuwa na nidhamu na heshima kwa wakubwa na wadogo ili kuleta ufanisi na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano.
Nape amesisitiza kupewa ushirikiano baina yake na naibu wake ili kuifanya wizara hiyo iwe wizara bora zaidi.
Aidha amesema kuwa wizara hiyo imekuwa ikipatiwa bajeti ndogo ukilinganisha na ukubwa wa majukumu yake huku akiahidi kuipigania katika vikao vya bajeti ili iongezwe na hivyo kutekeleza majukumu yake vilivyo.
Aliongeza kuwa atakuwa karibu na waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari kwa kuwa mlezi badala ya mtawala ili kutatua changamoto zinazowakabili.




Post a Comment