ad

ad

Majibu ya Davido kuhusu ujauzito wa Agnes Masogange!


Wiki moja iliyopita, Mtanzania Agnes Masogange alikuwa topic kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya post yake kwenye Instagram kuzua mjadala na kuibua uvumi mkubwa sana kati yake na Davido staa wa muziki kutoka Nigeria.
Masogange alipost kipimo cha ujauzito kwenye page yake ya Instagram, post iliyoibua mjadala mkubwa Nigeria na Tanzania na kuacha swali kubwa vichwani mwa watu, “Agnes ana ujauzito wa Davido?!”
maso4
Agnes Masogange.
Baada ya ukimya wa siku kadhaa, Davido aliamua azungumze na kuweka mambo sawa ili kusitisha uvumi unaosambaa juu yake na Agnes Masogange… kupitia page yake ya Twitter, Davido alipost tweets kadhaa huku akidai tetesi hizo zimemuumiza zaidi baada ya mrembo Masogange kumuendea hewani staa huyo kwa uchungu na kudai uhusiano wake na mpenzi wake upo matatani kutokana na uvumi huo.
maso2
Davido.
Haya ndio majibu ya Davido kuhusu uvumi wa Agnes Masogange kubeba ujauzito wake..
maso1
Powered by Blogger.