ad

ad

STARS MWENDO MDUNDO CHALLENGE CUP, YAKATA TIKETI KUCHEZA ROBO FAINALI


Timu ya taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’ imefanikiwa kuendeleza
ushindi kwenye mashindano ya Challenge yanayofanyika nchini Ethiopia, Kili Stars leo imeifunga Rwanda kwa magoli 2-1 kwenye mchezo wa pili wa kundi A uliopigwa kwenye mji wa Awasa.
Magoli ya Stars yamefungwa na Said Ndemla dakika ya 38 kipindi cha kwanza na Simon Msuva aliyefunga goli la ushindi dakika ya 76 kipindi cha pili.
Ushindi huo unaihakikishia Kili Stars tiketi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo huku ikiwa bado na mechi moja mkononi dhidi ya Ethiopia ambao ni wenyeji wa michuano hiyo.
Kilimanjaro Stars ilianza kupata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya Challenge dhidi ya Somalia kwa kuitungua kwa jumla ya goli 4-0 na leo pia wameitandika Rwanda kwa goli 2-1.
Powered by Blogger.