Arsenal kuaga kwenye Champions League leo?
Timu zilizofuzu: Real Madrid, Manchester City, Zenit
Timu ambazo zimeshatolewa: Borussia Mönchengladbach, Maccabi Tel-Aviv
Group E: Barcelona (10 points) v Roma (5), BATE Borisov (3) v Bayer Leverkusen (4)
Barcelona watapita na wataongoza kundi ikiwa tu watapata japo sare, lakini pia watafuzu hata kama watafungwa na Leverkusen ikashindwa kushinda.
Ikiwa BATE na Leverkusen watatoka sare, watakuwa nje ya nafasi ya kumaliza nafasi ya pili – ikiwa tu As Roma watashinda.
Group F: Bayern München (9) v Olympiacos (9), Arsenal (3) v Dinamo Zagreb (3)
Pointi moja tu itakuwa imetosha kuzihakikishia Bayern na Olympiakos kufuzu.
Bayern watakamata nafasi ya kwanza ya kundi, hata Olympiakos wanaweza kushika nafasi hiyo ikiwa watashinda kwa idadi ya magoli mengi ambayo itawapa faida ya head to head vs Bayern.
Arsenal wanahitaji kushinda huku wakiombea Olympiakos wapoteze ili waweze kuwa na nafasi ya kuwazidi mbio katika nafasi ya pili wakati watakapokutana nao katika mechi ya mwisho – Arsenal hawawezi kuwazidi Bayern.
Dinamo Zagreb wanahitaji kushinda na huku wakiombea Bayern wapoteze mechi ya leo ili wao waweze kuwafikia wakati watakapokutana katika mechi ya mwisho ya kundi jijini Zagreb – mechi ya kwanza walifungwa 5-0. Dinamo hawawezi kuwazidi Olympiakos.
Group G: Porto (10) v Dynamo Kyiv (5), Maccabi Tel-Aviv (0) v Chelsea (7)
Porto watafuzu endapo watapata tu sare. Watapata nafasi ya kwanza wakishinda na Chelsea wakipoteza au Porto akitoa sare na The Blues wakipoteza.
Chelsea watafuzu endapo watashinda na Dynamo Kiev watashindwa kupata ushindi.
Maccabi hawawezi kumaliza kwenye nafasi mbili za juu na ili wabaki kwenye kugombea nafasi ya 3 inabidi washinde na waombe Dynamo wafungwe.
Group H: Zenit (12, qualified) v Valencia (6), Lyon (1) v Gent (4)
Zenit wameshapita na watajihakikishia nafasi ya kwanza kwa kupata sare tu na hata kama wakipoteza bado head to head advantage itawabeba.
Valencia watafuzu ikiwa watashinda na Gent watashindwa kupata matokeo chanya.
Gent watapata katika top 3 na wataiachia Lyon nafasi ya 4 ikiwa watashinda au kupata sare ambao bado itawaeka mbele kwa takwimu za head to head vs Lyon.
Post a Comment