Ray C amekumbwa na aibu ya aina yake baada ya hivi karibuni...Tumekuwekea hapa

Imelda Mtema/GPL
Mwanamuziki
Rehema Charamila ‘Ray C’ amekumbwa na aibu ya aina yake baada ya hivi
karibuni kuvuja ‘video’ inayomuonesha akiwa mtupu huku akikata viuno.
Video
hiyo ambayo haimuoneshi uso lakini mkono wake wenye tatuu unaonekana
ilivuja kupitia ukurasa wake wa Instagram, jambo ambalo liliwafanya watu
washangae.
Katika
video hiyo anaonekana kama Ray C yuko faragha na ‘mtu’ wake na wakati
watu wakiendelea kuijadili, ilitolewa fasta kwenye ukurasa wake.
Hata hivyo, wakati ikitolewa, tayari wajanja walikuwa wameshainasa hivyo kusambaa kama moto wa kifuu.
Akizungumza na Ijumaa kuhusiana
na video hiyo, Ray C alikiri kuwa ni yake, ilikuwa kwenye simu yake
lakini aliibiwa na aliyemfanyia uhuni huo ni aliyemuibia.
“Ni
kweli ni yangu ila siyo mimi niliyeiweka kwenye ukurasa wangu wa
Instagram. Hiyo video ilikuwa kwenye simu yangu sasa imeibiwa na mtu
aliyeiba ndiye aliyenifanyia kitu hicho kibaya, hapa najipanga kwenda
polisi,” alisema Ray C.
CHANZO: IJUMAA GAZETI
Post a Comment