Wananchi wazidi kuibana Tigo
KUFUATIA
utetezi wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, juu ya kushindwa kutoa
huduma kwa wateja wake siku nzima ya Jumapili iliyopita, wananchi
wamezidi kuibana baada ya kauli iliyotolewa na shirika la umma la TTCL
kukanusha sababu zilizotolewa na Tigo.
Katika
taarifa iliyotolewa Jumatatu kwa vyombo vya habari, Tigo iliwaomba
radhi wateja wake kwa usumbufu uliotokea, wakisema ulisababishwa na
kukatika kwa mkongo wa taifa katika sehemu tofauti.
Katika
mahojiano na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa
wiki, TTCL ilisema kuwa kukosekana kwa huduma za Tigo siku hiyo
hakukutokana na kukatika kwa mkongo wa taifa, kwani kama ingekuwa hivyo,
mitandao mingine yote nayo ingesumbua, kwani yote hutumia mkongo huo wa
taifa.
“Tigo
waseme ukweli wa nini kilitokea siku ile, wana matatizo yao ambayo
hawataki kuyaweka wazi, kwa sababu suala la kusumbua kwa huduma zao ni
la kila mara, sasa kama mkongo ni mmoja na watumiaji ni kampuni zote,
kwa nini wao tu ndiyo wawasumbue wateja wao? Waseme kweli juu ya tatizo
lao tujue,” alisema mmoja wa wateja waliopiga simu chumba cha habari,
Tedds Wane wa Kibamba.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita watumiaji wa Mtandao wa Tigo walipata shida kubwa
baada ya huduma hizo kutopatikana tangu Jumapili asubuhi hadi alfajiri
ya Jumatatu, jambo lililowafanya wateja wengi kutaka taasisi hiyo
kuchukuliwa hatua na mamlaka za juu kwani ziliwapatia hasara.

Post a Comment