Hii sasa ni Fedheha! Msanii Bongo Avua Nguo Studio, Apiga picha za aibu
Msanii
wa muziki anayefahamika kwa jina la Rukia Jumbe ‘Rucky Baby’ amepata
fedheha ya aina yake baada ya kuvua nguo studio kisha kupiga picha za
nusu utupu.
Msanii huyo mrembo, alikumbwa na kadhia hiyo alipokuwa akipiga picha kwa ajili ya kujitangaza kutokana na kazi zake za kimuziki.
Chanzo
kilichovujisha picha hizo kilidai kuwa, awali msanii huyo alifika
kwenye studio moja iliyopo maeneo ya Msasani jijini Dar kwa lengo la
kupigwa picha lakini cha ajabu zilipigwa nyingi baadhi zikiwa za utupu.
“Alipomaliza
kupigwa zile picha, akapewa zote lakini ndani yake zilikuwepo picha
zake za nusu utupu, kwa hiyo akachagua za kupeleka kwenye vyombo vya
habari na mimi ndipo nikazinasa hizi chafu,” kilidai chanzo hicho
ambacho ni rafiki wa karibu wa msanii huyo.
Katika
picha hizo, msanii huyo anaonekana akivua shuka alilojifunga na
kumfanya abaki mapaja na matiti wazi, kitu ambacho ni kinyume kabisa na
maadili.
Katika kujua kulikoni msanii huyo apige picha hizo, mwandishi wetu alimtafuta na alipopatikana alisema:
“Jamani
hizo picha nilipiga studio lakini sikumbuki kama zipo zinazonionesha
nikiwa mtupu. Huyo mwanaume anayeonekana ni dairekta, alikuwa
akinielekeza jinsi ya kuweka mapozi tu,” alisema msanii huyo.
CHANZO: IJUMAA GAZETI - GPL

Post a Comment