Nay wa Mitego anasa kwa mrembo wa Marekani
MAHABA niue! Mkali wa ngoma ya Hip Hop,
Nyumbani Kwetu, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amenasa kwa mtoto
matata wa Kitanzania aishiye nchini Marekani ajulikanaye kwa jina la
Stella Tillya ‘Chagga Baby’.
Ubuyu kutoka katika chanzo chetu unasema
kwamba, kwa kipindi kirefu wawili hao wamekuwa katika uhusiano wa
kimapenzi lakini hawakuweka wazi mpaka pale penzi liliponoga na kuanza
kuandikiana posti za kimalovee katika mitandao ya kijamii hususan
Instagram.
“Kumbe mlikuwa hamjazinyaka? Mbona sasa
hivi ndiyo habari ya mjini! Shamsa tupa kule. Walianza kimyakimya mpaka
penzi lilipowanogea na kuanza kuliweka wazi,” kilisema chanzo kilicho
karibu na Nay.
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi na
kusema kwamba sasa hivi Nay haoni wala hasikii kwa mrembo huyo ndiyo
maana anajiweka wazi mpaka kwenye Mtandao wa Instagram.
Mara baada ya kupenyezewa ubuyu huo,
gazeti hili kupitia kachero wa kitengo cha OFM aliingia mzigoni na
kufanikiwa kubamba mawasiliano ya kimalovee kati ya Nay na Chagga Baby.
Mara baada ya kuweka kibindoni ushahidi
wa SMS kupitia kwa mtu wa karibu na Nay aliyeziiba katika simu yake,
gazeti hili likamvutia waya Nay ili atoe ufafanuzi wa penzi hilo kwani
hana muda mrefu tangu wamwagane na mwigizaji wa Kibongo, Shamsa Ford.
“Kaka usiwe na presha, hivi vitu vya ndani kabisa, vikiwa poa, kila kitu kitakuwa wazi,” alisema Nay.
Ikumbukwe kwamba kabla ya Nay kuzama
katika penzi la Chagga Baby, aliwahi kutoka ‘kimalovee’ na mrembo
aliyezaa naye, Siwema kabla ya kuangukia katika mikono ya muigizaji
Shamsha ambaye naye alimbwaga.

Post a Comment