Mh.James Lembeli amefungua kesi katika mahakama kuu kanda ya Shinyanga kupinga matokeo
Hatimaye aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo Chadema jimbo la Kahama mjini Mh.James Lembeli amefungua kesi katika mahakama kuu kanda ya Shinyanga kupinga matokeo ya kura za ubunge jimboni hapo katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 25 mwezi wa kumi mwaka huu.
Akizungumza baada ya kufungua kesi namba 1 ya uchaguzi mwaka 2015 iliyosajiliwa na naibu msajili wa mahakama hiyo Mh.S.P Mwaiseje, Mheshimiwa Lembeli amezitaja sababu zilimsababisha yeye mwenyewe kupitia chama demokrasia na maendeleo Chadema kufungua kesi ili kutetea haki ya wananchi wa jimbo la Kahama mjini.
CHANZO: ITV
Post a Comment